Mzee Kipingi

ilizaliwa miaka 57 iliyopita huko
tosa maganga iringa ,Mwaka 1985
hadi December 1987 nilikua mwanafunzi
wa kwanza Mwanzilishi wa shule hapa
oysterbay ikijulikana kama Oysterbay
technical school iliyoanzioshwa na jimbo
kuu la Dar es salaam na kusimamiwa na
parokia ya St.peters . Mwl wangu aliitwa
Br. Bonaventura Malibicha wa shirika la
wabenedictine kutoka hanga monastery
songea na Mwl. Patric Hossah ,Licha ya
uanafunzi lakini pia nilikua mwalimu
msaidizi wa elimu ya ufundi.Mwezi
January 1988 niliajiriwa kua mwalimu
kamili wa shule hiyo ambayo ni hapa
Don Bosco Oysterbay.
Namshukuru mungu kwa kuanzishwa
shule hiyo licha ya kwamba tulikua na
karakana moja (Workshop) ,madarasa
Mawili ,ofisi moja na stoo mbili ,moja ya
mbao na nyingine ya kuifadhia
vyombo,Wanafunzi walikua ni fani ya
useremala tu wakiwa Mwaka wa kwanza
15 na mwaka wa pili 13 ,namshukuru
Mungu mwaka huu tuliweza kusajili shule
kwa jina hilo ob/dsm/103/88 pia Mwaka
huo tuliweza kufungua account ya shule
kutokana na shughuli za uzalishaji zilizokua
zikiendelea.Pia nashukuru sana jimbo
walinitia sana moyo kupitia kwa paroko na
Kerdinal wetu marehemu Rauliani Rugambwa
waliweza kufika mara kwa mara
kutuona maana eneo la shule lilikuwa
limezungukwa na vichaka vingi, Mwishoni
mwaka 1989 baada ya mazungumzo
ya kuwaomba wasalesian wa mtakatifu
Don Bosco kuja kuendesha shule hii
hatimae Osterbay technical school ilikabidhiwa
kwa Wasalesian wa Bon Bosco
Mwezi November 1989 , Makabidhiano
yalifanyika office ya kanisa la mt Petro
oysterbay,baina ya wakili wa Mt petro
ambao ni Marehemu Fr. Juvenalis Muba
aliekua paroko wa Kanisa hilo,mimi
Mwenyewe .Mwl patric hossa ambae
Mwaka uliofuata alistaafu ,Mwakilishi wa
Don Bosco alikua Padri. Peter Poul rector
wa Don Bosco Upanga ,wakati huo mimi
pia nilikabidhiwa kwa shirika hili la wasalesian
wa mt.yohane bosco. Mwaka 19
shule ilimpata rector /gombela wa
kwanza. Fr. Mathew Punthumeana kutoka
upanga,ujio wake
ulianza kuzaa matunda sana kwani shule
ilizungushiwa ukuta na tulifanikiwa kujenga
nyumba ya mapadri kwakuwa mapadri
walilazimika kutoka
hadi leo .ninazo sababu kuu mbili juu ya
uwepo wangu hapa. Kwanza,Niliahidi
mbele ya Mwadhama kardinali Lauriano
Rugambwa marehemu astarehe kwa
amani,kuwa maisha yangu yote ni kwa ajili
ya vijana .naomba mu ngu anisaidie niwe
mwaminifu hadi nguvu zitakapo niishia
niendelee kuwepo Don Bosco.
Pili ,ninapenda sana mfumu kinga wa
malezi ya Don Bosco kwa vijana.Nina
onja upendo wa pekee kwa Baba Yohane .
Hitimisho kulinganisha na miaka ya
nyuma ,maendeleo yamekua mengi sana
hapa Oysterbay vtc, namshukuru sana Fr.
Babu Augustine kwa juhudi zake kwa jumuiya
yetu,kila mmoja akitimiza wajibu
wake ipaswavyo atasaidia sana kuwa njia
ya mafanikio kiroho na kimwili.umekua na
juhudi zinazoonekana kwa kuwapa vijana
maadili pamoja na juhudi masomoni na
hata makazini.ubarikiwe sana baba padre.
“Naomba niwashukuru wakuu
wangu wote niliofanya
nao kazi
Don Bosco,siwezi kuwataja
wote
Mungu Ibariki Don Bosco.”
-Mwalimu Pancras Joseph Nalembo Kipingi
Upanga na kuja kufanya kazi hapa ysterbay
,pia shule ya ufundi seremala upanga
iliyokua na
wanafunzi nane (8)iliunganishwa na ya
Oysterbay nakuleta idadi ya wanafunzi
36,pia tuliungana na mwl Elias msenji kutoka
upanga,ni vigumu kumsahau mwalimu huyo
kutokana na jitihada zake upande wa useremala.
Mwaka 1995 baada ya fr Methew kuhamia
huko makalala Iringa tulimpata
Br.Alfonso Morcel ,wakati huo ikumbukwe
tulikua na fani ya useremala tuu mwaka 1996
ujenzi wa workshop ya useremala mpya
ulianzwa na kukamilika
Tarehe 28 / 11 /1997. nawashukuru Don
Bosco chini ya usimamizi wa Masseno kwa
jitahada zao za kuendelea kutusaidia hatimae
fani ya useremala ilihamia jengo jipya kutoka
ilipkuwa welding kwa sasa,na
ikaazishwa fani mpya welding, Mwaka 1998
fani ya umeme ilifunguliwa rasmi mahali
zilipo ofisi za shule lilikuwa darasa moja na
mkuu wa chuo wakati huo aliitwa Br.
Stephen Jubejia na pia akiwa mwalimu wa
fani hiyo .
Nawashukuru sana wasalesian wa don bosco
kupitia watumishi hawa (Br.Alphonso na
Br.Stephen), Walijitahidi sana kuhakikisha
wana iinua shule hi mwaka 2000 uongozi wa
Don Bosco Oysterbay na shirika kwa ujumla
chini chini ya wasismamizi hawa walianza
ujenzi wa jengo lenye gorofa moja hatimae
jitihada zao zilizaa matunda na tarehe
31 /01 /2003 jengo liliisha na kuanza kutumika
rasmi .Fani ya umeme na computer
zilihamia kwenye jengo hilo ,pia fani ya
computer ilianzishwa maadam Bahati Lasway
na Marehemu Mshasha,mwaka uliofuata
2004 ilianzishwa fani ya uhazili (secretarial)
chini ya mwalimu Bahati Lasway .
Vilevile namshukuru mungu kwa zawadi ya
mkuu wetu wa chuo Fr.Babu Augustine na
wasaidizi wake kwan tangu wamefika hapa
tumebarikiwa sana ,fani zimeongezeka kama
ushonaji ,,ufundi wa magari ,solar(umeme wa
jua),na majengo toka workshop moja hadi 8,
madarasa 13 kutoka 1 , ofisi 12 , stoo 9 kutoka
na vyoo 23.Mungu awabariki sana.pia
nawashukuru walimu wote , Wafanyakazi
pamoja na wanafunzi wote walio shirikiana
nami kwa kipindi chote hadi sasa.Wengi
wenu mnaweza kua na maswali kwamba ni
kwanini nimeendelea kuwepo don Bosco