Interview with Mr Edward.

Mr. Edward Mundagele is the head of Carpentry Department and of the first past pupils Don Bosco Oysterbay.

Fausta: Habari ndugu ,kwa majina naitwa Fausta Ngatunga,mwandishi wa gazeti la chuo
Edward: mimi naitwa Edward Mundagele ni Meneja uzalishaji hapa katika chuo cha Oysterbay V.T.C.
Fausta: Je,unaweza kutuelezea kwa ufupi kabisa historia fupi ya maisha yako ya kikazi mpaka kufikia majukumu haya makubwa uliyonayo katika
chuo hiki?
Edward: Ndugu mwandishi. Kama nilivyoeleza awali Jina langu Edward Mundagele,nilijiunga hapa Don Bosco Oysterbay mwaka 1995; Ni baada ya kuhitimu
kidato cha nne mnamo mwaka 1991 katika shule ya sekondari ya kijeshi; Mirambo TPDF sec.school iliyopo mkoani Tabora. Mafunzo yangu ya ufundi seremala niliyapata hapahapa Don Bosco Oysterbay kwa muda wa miaka miwili,mwaka 1995/1996 na kufuzu mafunzo ya useremala katika Daraja la III. Mnamo mwaka 1998 nilisajiliwa kufanya mtihani wa Trade Test katika daraja la pili(II). Nilifanya nadharia na vitendo na kufaulu na kutunukiwa cheti cha Trade Test daraja la pili(II) katika fani ya useremala. Wakati huo 1997 nilikuwa tayari nafanya kazi kama fundi katika kipindi ch matazamio ya ajira ya muda,chini ya uangalizi wa mwalimu Elias Msenji ambaye alikuwa Workshop Manager wakati huo na mwalimu Pancras Kipingi mkuu wa chuo pia Admnistrator alikuwa Br. Alfonso.
Fausta: Unaonaje kazi ya uzalishaji wa samani na shughuli zote za useremala katika karakana yenu kwa nyakati hizo ukilinganisha na nyakati hizi.
Edward: kwa kweli kwa nyakati hizo uzalishaji ulikuwa mdogo sana, na hali hiyo ilichangiwa na uchache wetu, udogo wa karakana na uchache wa zana za kufanyia kazi. Kwa vile tulikuwa mafundi wasaidizi wawili, mimi Edward Mundagelena Mr. Godfrey Mwangaline na walimu wawili mwl,Pancras Kipingi na Mwl.Elias Msenji,jumla ni wane tu.
Fausta: Ni hatua zipi zilichukuliwa ili kukabiliana na changamoto hiyo?
Edward: Uongozi ulipata mashine mpya kwa lengo la kuongeza uzalishaji; Hivyo basi uongozi uliazimia kupata mafundi walio na ujuzi wa kuzitumia mashine hizo. Hivyo basi mimi na mwenzangu Godfrey tulipelekwa Embu-Kenya ili kupata mafunzo ya jinsi ya kuzitumia mashine hizo. Mafunzo yalichukua muda wa miezi sita (6), na tulitunukiwa cheti kwa mafunzo hayo.Baada ya mafunzo hayo, kazi zilifanyika kwa ufanisi zaidi,uzalishaji ukaongezeka. Mwaka uliofuatia 1998 uongozi uliamua kuwapeleka mafundi wengine kwenda kusoma Embu-Kenya. Hawa ni wahitimu wa Don Bosco-Oysterbay waliofanya  vizuri, ndipo Mr. Frank Kihiwili na Mr. Daniel Ulungi walipelekwa pia. Baada ya mafunzo yao; uongozi ulikuwa na utaratibu wa kupata mafundi toka kwa vijana wetu, wanaohitimu na kufanya vizuri,walifundishwa lakini changamoto kubwa ni kwamba wanaondoka na kufuata maslahi bora zaidi.
Fausta: Je,utaratibu huo wa kuchagua wahitimu wetu bado unaendelea nani wangapi tunao mpaka sasa?
Edward: kwasasa utaratibu huo haupo;mara ya mwisho kuwepo utaratibu huu ilikuwa mwaka 2007 ambapo wavulana ni wawili, lakini waliacha kwa nyakati tofauti. Walichaguliwa wahitimu watano 5 kati yao watatu ni wasichana ambao tunao hadi hii leo; Claudia Jackson, Ms Odetha Raphael ambao bado wanatumikia karakana ya useremala na Ms. Theresia Kisompo ambaye amepangiwa jukumu la ukutubi katika maktaba ya chuo.Na hawa ni wanafunzi wa kwanza wa jinsia ya kike kufanya kazi katika karakana ya useremala Oysterbay na kwa kweli wanachapa kazi.
Baada ya hapo, uongozi ulipobadilika utaratibu huo haukuendelea tena .
Fausta: Je unaweza kutueleza mafanikio yoyote au hata changamoto kama zipo?
Edward: Nikianzia na mafanikio, Kutokana na ufanisi katika kazi zetu, ufanisi huo umekitangaza chuo chetu na kutambulika zaidi. Chuo kimeweza kutoa mafundi wengi sana na waajiri wengi wanahitaji mafundi kutoka Don Bosco.
Taasisi nyingi za kidini na makanisa wanatengenezewa samani zao Don Bosco Oysterbay. Uzalishaji umekuwa ukiongezeka katika nyakati za hivi karibuni, katika mafanikio mengi changamoto hazikosekani. Uzalishaji umekuwa ukipungua katika nyakati za hivi karibuni kutokana na upungufu wa wateja. Mafundi
wazuri wanapoondoka, inapelekea kupungua kwa wateja na uzalishaji pia.
Kumekuwa na tatizo la upatikanaji wa mbao kavu hasa wakati wa masika na kupelekea kuchelewa kukauka. Wauzaji wengi hushindwa kuhifadhi mbao ili wauze zikiwa kavu; hivyo mbao hukaushwa na sisi wenyewe.
Fausta: Ni nini maoni yako?
Edward; Iko haja ya kuanza kusajili wanafunzi wengi tuwashawishi ili wapende kujiunga na fani ya useremala na hatimaye wamalizapo mafunzo wengine wabaki hapa chuoni ili kuondokana na changamoto ya mafundi wazuri wanapoondoka kupungua kwa uzalishaji.