WELDING & FABRICATION

Fani ya uchomeleaji yaani welding & fabrication imeanzishwa rasmi
mwaka 1998 viongozi wakiwa Ni Br. Steven Jubeja Adminstrator na
Br. Alfonso, Mwalimu wa welding alikuwa ni ndg Peter Mpululu.
Welding & fabrication tumekuwa tukipokea kazi mbalimbali za kila
aina ya chuma Kama vile mageti, magrili, viti, madawati, makabati, mapaa
ya nyumba, milango, magari na vitu vingi vinavyohusiana na chuma. Tumekuwa
tukufanya kazi Kwa bidii na kujituma pamoja na kumshirikisha
Mungu kwa kila hatua tunayo pitia na pia kumshukuru Mungu kwa
viongozi bora anao tupatia. Wateja wanatukubali kwa kazi zetu bora na
zenye kuvutia, tumekuwa tukifanya kazi za makanisani, makampuni na
nyingine nyingi za watu binafsi. Ufanisi wa hali ya juu na jinsi tunavyofundisha
vijana. Nyuma tulikuwa tunasoma masomo mawili tu ambayo ni
nadharia na vitendo Kwa mfumo wa CBET tulikuwa tukitoa mafundi bora
na ndio wanao ijenga Tanzania yetu kwa sasa,Tulifundisha vijana jinsi ya
ufanyaji kazi na jinsi tunavyofanya uchomeleaji pia kukimbizana na soko
la samani na bidhaa mpya zinazoingia sokoni kulingana na utamaduni.
Ninachokijua ni kwamba kila kazi ina changamoto zake kikubwa ni
kumshukuru Mungu mpaka sasa tupo na huu ni mwaka wa ishirini (20)
toka mwaka 1998-2018 .Kingine napenda kusema ahsante kwa uongozi wa
sasa kufanya kazi vizuri. Fr. Augustine Babu,Fr. Peter Mutechura na Br.
Jose Kappanannaickal .Mwenyezi Mungu Awabariki na pia tunapenda kuwatakia
maisha marefu ya hapa duniani pia mzidi kuwalea vijana katika
utume mwema na malezi yaliyo bora.