Secretarial Course

Duration 2 years

Idara ya uhazili (secretarial) ilianzishwa mnamo mwaka
2004 chini ya uongozi wa Fr. Joseph Madapally (M.C. Jose).
Ilianza na wanafunzi 10. Mwalimu mwanzilishi alikuwa
madam Agatha Lasway. Alifundisha kwa muda wa miaka 5
(mitano) na kuhamia idara ya computer. Awamu ya pili iliongozwa
na marehemu mwalimu Boniface Muhonda kwa
muda wa miaka 3 hatimae akastaafu kazi. Awamu ya tatu iliongozwa
na madamu Helen Jackson Kalindimya kuanzia
mwaka 2009 anaendelea mpaka hii leo. Fani hii ilikuwa ikifundishwa
kwa muda wa mwaka 1 (mmoja) ambapo ilianza
na masomo ya fani ambayo ni
Walimu wengine waliowahi kuhudumu ni kama; mwalimu
Stephen Maile na Madamu Agatha Lekule. Fani hii ina uhaba
wa wanafunzi wa kiume. Mara zote imekuwa ikipata wanafunzi
wa kike tu. Pamoja na hayo fani hii ni ya jinsia zote.