Computer Department

We offer Veta approved courses. Computer packages are available for anyone.

Idara ya computer ilianza rasmi mwaka 2003 chini ya uongozi wa Fr Joseph
Madaphly ndiye aliyekuwa mkuu wa chuo na bwana fedha ambaye ni Marehemu
Br Alphonso. Idara ilianza na walimu ambao ni Madam Bahath Agatha
Lasway na Marehemu Filbert Mshasha. Idara ilianza ikiwa na LAB mmoja, computer
zipatazo 22, scanner 1. na Printer 3.
MADHUMUNI
Madhumuni ya kuanzisha course ni kuwasaidia watu wote wa rika tofauti
waweza kuendana na tecknologia ya sasa. Pia kujiwezesha katika swala zima la
ajira.
Idara ya computer ilianza na idadi ya wanafunzi wapatao 45 ambao walikuwa
wanatoka nje ya chuo wanaotambulika kama short course, kipindi hicho wanafunzi
wa V.T.C. hawakuwa na fursa ya kusoma computer.
kadiri tecknologia ilivyozidi kukua wanafunzi waliongezeka na idara ya computer
ilikuwa zaidi na kuongeza program mbalimbali kama
Mnamo mwaka 2009 chini ya Uongozi wa Br Francis Muli na Fr Eric waliongeza
lab nyinge pamoja na projector moja ikiwepo na smartboard kwajili ya kufundishia
,na wanafunzi wa V.T.C. walianza rasmi somo la computer kwa kila fani.
Kuulingana na uhitaji wa technologia idadi ya wanafunzi iliongezeka na kufikia
kiwango cha juu. Kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi, Uongozi ulichukua
jukumu la kuongeza idadi ya vitendea kazi kama vile, computer, scanner, printer
etc. computer ziliongezeka na kuwa na idadi ya computer zipatazo 40.
Tunashukuru kwa Ungozi wa sasa kwa hatua nzuri ya undeshaji wa Chuo ambao
umeweka jitihada kubwa katika kukiendeleza Chuo chetu.