Fitter Mechanics

Karakana ya fitter mechanics ilianzishwa na Alfonso Morcelli
mwaka 2003 kwa malengo ya kuwasaidia wanafunzi kupata elimu
ya ufundi wa uchongaji vipuri pamoja na kufanya uzalishaji wa
kazi nje .
Mwaka 2003 mwezi wa 3 aliwasili mwanafunzi anayeitwa Essau Alex
kwa lengo la kusaidiana na Br Alfonso mercell akitokea chuo cha ufundi
Dodoma, Mwaka 2004 Mr.Emanuel kapama (mwanafunzi wa DB Dododma)
alijiunga kwa kazi ya ufundishaji na uzalishaji. Mwaka 2005
alikuja mkuu wa chuo mwingine Br. Celestine baada ya Yule wa awali
kuhamishwa kwa hiyo alipofika mwaka 2006 tulianza rasmi kufundisha na
kupokea wanafunzi kwa ajili ya kujifunza . Tuli anza na wanafunzi wawili
tu( Boniface mwami na Lurent Charles) ambao walihitimu mwaka 2007
kwa ufaulu mzuri. wanafunzi walikuwa wakiongezeka kila mwaka kutokana
na ubora wa walimu pamoja na vifaa vya kufundishia na mashine
mbalimbali lakini pia uongozi bora wa vipindi tofauti tofaut ,Mpaka hivi
leo 2018 bado tungali tunaendelea. Tulikuwa na wanafunzi wa katika ngazi
tatu, yani mwaka wa kwanza wa pili na wa tatu. kwa sasa tuo chini ya
uongozi wa Fr. Babu Augustino ambaye kwa sehemu yake ameweza kutuongezea
waalimu wa power saw ( kukata vyuma) mbalimbali kwa ajili
ya kazi.hii imesaidia sana katika ufundishaji pamoja na
uzalishaji.tunamshukuru san kwakuliona hili.
Ninawashukuru sana wasalesian wote wa Don Bosco ingawa wengi wao
walishaondoka kuendelea na majukumu mengine ya ujenz wa taifa mungu
awabariki sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *