Welding, Metal Fabrication

Duration 3 years

Welding, Metal Fabrication and Aluminum course-Level III Certificate CBA:
Students learn metal works, how to fabricate different types of metal works and aluminum
work in theory, and practical and Technical Drawing. They also participate in production of windows, door grills, and other metallic products.

HISTORIA

Fani ya uchomeleaji yaani welding & fabrication imeanzishwa rasmi
mwaka 1998 viongozi wakiwa Ni Br. Steven Jubeja Adminstrator na
Br. Alfonso, Mwalimu wa welding alikuwa ni ndg Peter Mpululu.
Welding & fabrication tumekuwa tukipokea kazi mbalimbali za kila
aina ya chuma Kama vile mageti, magrili, viti, madawati, makabati, mapaa
ya nyumba, milango, magari na vitu vingi vinavyohusiana na chuma.
Tumekuwa tukufanya kazi Kwa bidii na kujituma pamoja na kumshirikisha
Mungu kwa kila hatua tunayo pitia na pia kumshukuru Mungu kwa viongozi
bora anao tupatia. Wateja wanatukubali kwa kazi zetu bora na zenye
kuvutia, tumekuwa tukifanya kazi za makanisani, makampuni na nyingine
nyingi za watu binafsi. Ufanisi wa hali ya juu na jinsi tunavyofundisha
vijana. Nyuma tulikuwa tunasoma masomo mawili tu ambayo ni nadharia
na vitendo Kwa mfumo wa CBET tulikuwa tukitoa mafundi bora na ndio
wanao ijenga Tanzania yetu kwa sasa,Tulifundisha vijana jinsi ya ufanyaji
kazi na jinsi tunavyofanya uchomeleaji pia kukimbizana na soko la samani
na bidhaa mpya zinazoingia sokoni kulingana na utamaduni.
Ninachokijua ni kwamba kila kazi ina changamoto zake kikubwa ni
kumshukuru Mungu mpaka sasa tupo na huu ni mwaka wa ishirini (20)
toka mwaka 1998-2018 .Kingine napenda kusema ahsante kwa uongozi wa
sasa kufanya kazi vizuri. Fr. Augustine Babu,Fr. Peter Mutechura na Br.
Jose Kappanannaickal .Mwenyezi Mungu Awabariki na pia tunapenda kuwatakia
maisha marefu ya hapa duniani pia mzidi kuwalea vijana katika
utume mwema na malezi yaliyo bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *