Electrical

Fani ya Umeme ilianzishwa hapa Don Bosco Oysterbay
mwaka 1998 ikiwa na wanafunzi 8, mwalimu wa kwanza
kufundisha shule hii alikuwa Mkuu wa chuo wakati huo
ambae pia ni Brother wa shirika la Mtakatifu Yohani Bosco
anaitwa Brother Stephen Geobegia ambae ni raia kutoka Italy.
Tunamshukuru sana huyu brother kwani aliweza kufanya kazi
nyingi sana kama Mkuu wa chuo lakini pia kama mwalim. Fani
hii ilianzishwa mahali ambapo zipo ofisi za shule, ofisi zote tatu
llikuwa ndio Darasa Moja la umeme.mwaka uylio fuata 1999
Mkuu wa shyule alikwend itali akiwa huko aliweza kufany mipango
mbalimbali ambao mwaka 2000 tulifanikiwa kupata vifaa
mbalimbali Makontena mawili kwa ajili ya kutunzia vifaa ambavyo
tuna shukuru mbaka leo vina tusaidia sana hapa chuoni
kwaajili ya kufundishia na pia kweanye matengenezo mbalimbali
katika kituo chetu Mwaka 2002 idara ya umeme ilifungu liwa
rasmi kwenye jengo mahali ambayo idara hi ipo . Baadhi ya
walimu walio fundisha idara hii ni Mwalimu Thobias kaduma ,
Mwalimu Patric Mhemera , mwalimu Tairo na sasa Mwalimu
Geoffrey Nangeda na Mwalimu Abelli Kifela tuna washukuru
wote kwa kazi nzuri walizo fanya na wanazo endelea kufanya
katika kuleta maendeleo katika chuo chetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *